Kifo cha Rais Mkapa, Yanga yasema imepoteza nguzo muhimu

0
264

Kufuatia kifo cha Rais Benjamin Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia Julai 24 mwaka huu, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema klabu hiyo imepata pigo kubwa kwa kumpoteza mwanachama wake.

Akizungumza na TBC, Dkt. Mshindo Msola amesema msiba huo umegusa makundi mbalimbali ndani na nje ya nchi ukiwemo uongozi wa klabu ya Yanga.

Msola ameongeza kuwa klabu hiyo imepoteza mshauri mkubwa katika masuala mbalimbali yaliyokuwa yakihusu maendeleo ndani ya klabu hiyo.

Amewataka wanachama na mashabiki wote wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuaga mwili wa kiongozi huyo.