KIAPO KWA MBUNGE MPYA

0
124

Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akimuapisha Mbunge wa Viti maalum CCM Tamima Haji Abass kuwa Mbunge baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Julai 9 mwaka huu kuchukua nafasi ya aliyekuwa mbunge wa viti Maalum Irene Ndyamkama aliyefariki Dunia.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimkaribisha Bungeni Mbunge mpya wa Viti maalum CCM Tamima Haji Abass, ambaye ameapishwa hii leo kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum Irene Ndyamkama aliyefariki dunia Aprili 24 mwaka huu.