Kemeeni mmomonyoko wa maadili

0
121

Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa amewahimiza Viongozi wa dini na wananchi wote kukemea mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii.

Akizungumza katika Baraza la Eid Al Adha kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI Kinondoni, Dar es Salaam Waziri Mkuu amewataka viongozi wa dini kutumia nafasi zao kila wanapozungumza na waumini wao kuwahimiza kuzingatia maadili mema na utamaduni wa Kitanzania.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kudhibiti uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi ambavyo ni sehemu ya mmomonyoko wa maadili.

“Tumejitahidi kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya kutoka nje ya nchi kuja ndani kwa kuweka vituo maalumu vya ulinzi kwenye maeneo yote yanayofikiwa na abiria; bandarini vituo vya mabasi, maeneo ya viwanja vya ndege na maeneo yote yenye mikusanyiko ili kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya”. amesema Waziri Mkuu