Katika kuendeleza ushirikano wa kiutamuduni kati ya China na Tanzania, kituo cha utamaduni cha nchi hiyo hapa nchini kimeandaa tamasha litakalowakutanisha wadau wa michezo na utamaduni kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 5 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuboresha ushirikiano.
Tamasha hilo linakwenda sambamba na kusherehekea sikukuu ya mwezi wa kichina na mwaka mpya wa kichina ambapo waandaaji wa tamasha hilo kupita afisa utamaduni wake Ye Tianfa amesema washiriki watapata nafasi ya kujifunza tamaduni mbalimbali za kichina ikiwemo lugha, chakula na michezo.
Kutokana na janga la COVID – 19 tamasha hili litafanyika kwa njia ya mtandao kwa waliopo nje ya Tanzania na waliopo jijini Dar es Salaam watahudhuria tamasha hilo katika sehemu itakayopangwa.