Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewahakikishia Wasanii nchini kuwa kazi zao za sanaa zipo salama.
Akizungumza wakati wa Tamasha la Sanaa la Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, Waziri Mwakyembe amesema, Kamati ya kusikiliza haki za Wasanii itaanza tena kusikiliza kesi za madai mbalimbali ya Wasanii ambao haki zao zimepotea kutokana na kuingia kwenye mikataba mibovu.
