Kazi ya kwanza kwa Balozi Kattanga

0
546

Balozi Hussein Kattanga ameapishwa hii leo na kuanza kazi papo hapo kwa kusimamia kiapo kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa kuongoza wizara mbalimbali.

Balozi Kattanga awali alikua Balozi wa Tanzania nchini Japan, na kabla ya hapo alikua Katibu Mtendaji wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Balozi Kattanga amewahi pia kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.