Zaidi ya Kaya Mia Mbili wilayani Babati mkoani Manyara hazina makazi, baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Babati, – Elizabeth Kitundu ametembelea maeneo hayo yaliyozingirwa na maji na kusema kuwa, nyumba Kumi zimebomoka kabisa na nyingine Kumi zimeezuliwa paa kufuatia mvua hizo.