Kawaida aahidi makubwa UVCCM

0
115

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,
Mohamed Ali
Mohamed maarufu Kawaida, ameahidi kuuimarisha umoja huo ili uzidi kuwa imara zaidi.

Kawaida ambaye amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM uliofanyika mkoani Dodoma amesema vijana ndio mtaji wa chama, hivyo ni vema UVCCM ikazidi kuimarishwa.

Mohamed Ali Mohamed ambaye kabla ya kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa alikuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Kusini Unguja, amechaguliwa kwa
kura 523 za ndio zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo.

Anachukua nafasi hiyo ambayo ilikuwa wazi baada Kheri James aliyekuwa akishikilia wadhifa huo kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam mwezi June mwaka 2021.

Rehema Omary yeye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kwa kura 416 za ndio.

Mkutano huo mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi pia umewachagua Wajumbe watatu wa halmashauri Kuu NEC kutoka UVCCM kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar na Wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Uchaguzi huo ulisimamiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.