Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Mashinji ajiunga CCM

0
346

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt Vicent Mashinji ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Dkt Mashinji ametangaza uamuzi huo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumunba jijini Dar es salaam na kupokelewa na Katibu wa NEC -Itikadi na Uenezi Humprey Polepole.

Amesema kuwa, ameamua kujiunga na CCM baada ya kukaa na kutafakari kwa kina na kuona chama hicho ndicho chenye nia ya dhati ya kuwaletea Watanzania maendeleo.