Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amesema wameokoa zaidi ya shilingi Milioni 52 fedha ambazo makarani wa ununuzi na upimaji wa pamba walikuwa wamezikusanya kutoka kwa wakulima bila ridhaa ya wakulima.
Homera amesema fedha hizo tayari zimekusanywa kutoka kwa makarani hao ambao moja kwa moja walikuwa wanawaibia wakulima wa Pamba