[4:31 AM, 12/27/2019] Hamisi Holela TBC: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ametangaza kuwashirikisha machifu na watemi mkoani humo ili kuhamisha mimba za wanafunzi kwenda kwa mwanaume waliosababisha wanafunzi hao kupata mimba
Homera ametoa kauli hiyo katika Kijiji cha Mwese wilayani Tanganyika na kuongeza kuwa kiwango cha mimba za utotoni hakijawahi kupungua mkoani humo.
Amesema machifu wa Kibende, Kipimbwe na Kikonongo watasaidia kuhamisha mimba hizo kutoka kwa wanafunzi hadi kwa wanaume waliowapa mimba wanafunzi hao.
Mwandishi Hosea Cheyo