Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lililopo ndani ya uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl. J.K Nyerere yanapofanyika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, na kutia saini kwenye ukuta maalum wenye saini za wahitimu mbalimbali waliotembelea banda hilo.
Waziri Mkuu alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.