Kasekenya: Ujenzi wa miundombinu usilete kero

0
120

Naibu Waziri wa Ujenzi wa Uchukuzi Mhandishi Godfrey Kasekenya amewataka wasimamizi na wakandarasi waliopata dhamana ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka hatua ya nne kutokuwa kero kwa kusababisha msongamano wa vyombo vya moto wakati wakiendelea na ujenzi.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka Mhandisi Kasekenya amewataka wakandarasi hao kuandaa mpango na utaratibu mzuri ambao hautaathiri shughuli za Wananchi na watumiaji wa barabara ambazo zimepitiwa na mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu kama Mwendokasi.

“Dar es Salaam ni mji ambao uko very busy, ukimpotezea mtu saa moja au saa mbili unakuwa umemkwamisha. Kwa hiyo muwe na mpango mzuri kuhakikisha kwamba katika ujenzi wa hizi barabara hamtengenezi misongamano isiyo ya lazima.” amesema Mhandisi Kasekenya