Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Amani Abeid Karume ambaye ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais pia amemteua Anne Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.