20 Juni ni siku ya wakimbizi duniani ambapo Tanzania imeungana na dunia nzima kuadhimisha siku ya wakimbizi duniani ikiwa na Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Hatua na wakimbizi”
Wapo wengi waliokimbia makazi yao sababu ya migogoro na vita katika nchi zao na kuwa wakimbizi katika nchi jirani.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola ametoa onyo kwa baadhi ya watu wanaowatia hofu wakimbizi hapa nchi kuhusiana na mataifa wanaoyotoka waache kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani iliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHRC na kuongeza kuwa serikali kamwe haiwezi kulifungia macho uchochezi huo unaofanywa na baadhi ya watu.
