Kandonga wa ITV afariki dunia

0
137

Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV na Radio One mkoa wa Songwe, Gabriel Kandonga amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi kwenye eneo la Karasha mji mdogo wa Mlowo.

Habari kutoka mkoani Songwe zinaeleza kuwa, wakati ajali hiyo inatokea Kandonga alikuwa kwenye gari binafsi na mwenzake Haika Sanga ambaye ni mwandishi wa habari wa Clouds TV..

Kwa sasa Haika anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Songwe baada ya kujeruhiwa katika ajali hiyo.