Kampuni ya ununuzi wa parachichi kufutwa

0
235

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameagiza kufutwa kwa kampuni ya ununuzi wa parachichi ya Kandia Fresh na kufungiwa kibali, kwa madai ya kuhusika na parachichi zilizotupwa dampo wiki mbili zilizopita mkoani Njombe.

Bashe ametoa agizo hilo akiwa katika kituo cha kuhifadhi parachichi cha kijiji cha Nundu mkoani Njombe, ambapo pia amekutana na msimamizi wa kampuni hiyo David Baraza na kuagiza ashikiliwe.

Pia amepiga marufuku wakulima kuuza parachichi ambazo hazijakomaa, kwa kuwa zinaua soko la parachichi la Tanzania Kimataifa na kuwataka viongozi wa mkoa wa Njombe kuwasimamia wakulima ili waache kuuza parachichi kiholela.