Kampeni ya ELIMISHA KIBAHA yazinduliwa

0
554

Wilaya ya Kibaha iliyopo mkoani Pwani imezindua kampeni ijulikananyo kama ELIMISHA KIBAHA ambapo wadau mbalimbali wa elimu watachangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba Sitini na Vitano vya madarasa.

Mkuu wa wilaya ya Kibaha, –  Assumpter Mshama amewaambia Waandishi wa habari kuwa wilaya hiyo inahitaji zaidi ya  Shilingi Bilioni Moja kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo Sitini na Vitano vya madarasa pamoja na kununua viti na meza.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha Mjini Jenipher Christian na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kibaha Mji Butamo Ndaluhwa wamewaomba watu mbalimbali kujitokeza  ili kuchangia fedha hizo.

Kampeni ya ELIMISHA KIBAHA itahitimishwa Julai Saba mwaka huu katika shule ya Sekondari ya Kibaha Boys ambapo watu mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara, Mashiriki ya umma pamoja na yale binafsi yameombwa kujitokeza kuchangia ili malengo yaliyowekwa yaweze kutimia.