ais Samia Suluhu Hassan amesema kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Serikali inakwenda kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Nchini ambapo kamera zitatumika katika maboresho hayo.
Rais Samia ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi.
Ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa magari mabovu yanayotembea barabarani, Jeshi la Polisi linakuja na mfumo wa ukaguzi wa lazima wa magari ambapo kila gari litatakiwa kukaguliwa.
Aidha, Rais Samia amesema Jeshi la Polisi litakuwa na mfumo wa utambuzi wa uchakataji wa taarifa za uhalifu ambao utasaidia kutambua mhalifu kwa njia ya picha, hivyo kulirahisishia jeshi hilo kufanya uchakataji wa taarifa za wahalifu.