Kamanda Nyigesa arudishwa makao makuu kupisha uchunguzi

0
254

Jeshi la Polisi nchini limefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Waliohamishwa ni aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Wankyo Nyigesa ambaye amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, William Mwampagale.

Aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Rukwa, Theopista Mallya anakuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kuchukua nafasi ya William Mwampagale ambaye amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera.

Aidha aliyekuwa Mkuu wa Operesheni mkoa wa Rukwa Mashenene Mayila anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa huo.

Uhamisho huo umefanyika ili kupisha uchunguzi wa tukio la tarehe 26 mwezi huu la kumuaga aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa ambapo alitoa maneno yanaonyesha kuwepo kwa ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya jeshi la polisi.