Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini FORTUNATUS MUSLIM amewataka madereva wa mabasi yaendayo mikoani kusitisha mgomo uliotarajiwa kufanyika hapo kesho na badala yake wafanye kazi yao kama kawaida.
Kamanda MUSLIM ameyasema hayo jijini DSM katika mkutano na waandishi wa habari na kuongeza kuwa taarifa za mgomo huo wamezipata na kuzifanyia kazi na kwa kuwa suala hilo tayari limefikishwa Mahakamani hivyo ni vyema madereva waache mahakama itoe maamuzi.
