Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, – Fortunatus Musilimu amesema jeshi hilo linafanya operesheni ya kuwasaka Wamiliki wa nyumba za kulala wageni, ambazo zinatumika kufanya biashara haramu ya watu kuuza miili maarufu Kama wadada na wakaka poa.
Kamanda Musilimu ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi na Viongozi wa kata ya Mafisa Manispaa ya Morogoro na kuongeza kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya watu ya kuwepo kwa nyumba za kulala wageni kujihusisha na biashara hiyo huku Wamiliki wakitajwa kuwa ndiyo chanzo.
Amesema mfanyabiashara ambae atabainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuwa fundisho kwa wengine.