Kagame kuwa na ziara ya siku mbili nchini

0
533

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Paul Kagame wa Rwanda anatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamis Machi saba kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Rais John Magufuli na inatarajiwa kutoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Halikadhalika viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kagame anatarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kesho alasiri na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais Magufuli.