KAGAIGAI: ELEKEZENI NGUVU KUIJENGA TBC

0
139

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Steven Kagaigai amewakumbusha wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa shirika hilo kuhusu umuhimu wa baraza hilo akisisitiza kuwa baraza la wafanyakazi linapaswa kuwa daraja kati ya mwajiri na waajiriwa ili kutekeleza jukumu kubwa la kuwa kiunganishi badala ya kitenganishi kwa kuwa mabaraza ya wafanyakazi yalitengenezwa ili kutekeleza misingi ya utawala bora.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano wa pili wa baraza jipya la wafanyakazi wa TBC, Kagaigai amesema n iwakati wa wafanyakazi wa shirika hilo kuelekeza nguvu zao kulijenga shirika katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Tanzania inaelekeza jicho katika kuboresha shirika hilo.

Mkutano wa baraza hilo unaojadili mpango na mwelekeo wa shirika hilo kwa mwaka 2023 umehitimishwa leo na mgeni rasmi wa baraza hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji (TBC), Stephen Kagaigai.