Nilipoteuliwa sikujua TBC ni kubwa hivi – Kagaigai

0
421

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Steven Kagaigai amesema hakuwa anaujua ukubwa wa TBC hadi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipomteua kuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo.

Kagaigai amesema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo cha kurusha matangazo ya redio cha TBC Taifa na TBC FM kilichopo Inyonga, Mlele mkoani Katavi

“Sikuwahi kujua kwamba TBC ni kubwa kiasi hiki na sikujua kuwa TBC inauwekezaji mkubwa kiasi hiki, baada ya kuteuliwa na kuzungushwa katika maeneo mbalimbali ndio nikagudua ukubwa wa TBC na nina uhakika wapo Watanzania wengi ambao hawajui kama TBC ni kubwa namna hii, matangazo yanakuja kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa taarifa nilizopewa alisema ataisaidia TBC na kwa kweli wote tunaona mpaka Mlele mnapata taarifa kupitia TBC,” amesema Kagaigai.

Hata hivyo, Kagaigai amesema kupitia uwekezaji huo mkubwa unaofanyika bodi ya TBC kwa kushirikiana na menejimenti ya TBC watahakikisha wanasimamia kuhakikisha Watanzania wanapata usikivu wa redio za TBC.