Kadhi Mkuu na Naibu Kadhi Mkuu waapishwa

0
194

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewaapisha Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali pamoja na Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Othman Ame Chum, kufuatia uteuzi alioufanya kwa hivi karibuni.

Hafla ya kuwaapisha viongzi hao wa dini imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuapishwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali amewataka wananchi wa Zanzibar kujenga ushirikiano na nahakama ya kadhi ili kuiwezesha kufikia utoaji wa maamuzi ya haki.