JPM: Siku tatu za kufunga na maombi

0
162

Rais Dkt. John Magufuli ametangaza siku tatu za kufunga na kuomba zinazoanza leo Ijumaa hadi Jumapili kwa wananchi wote kuliombea Taifa dhidi ya maradhi yanayoisumbua dunia kwa sasa.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Watanzania kuondoa hofu na badala yake kuchukua tahadhari na kumtanguliza Mungu.

Rais Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa serikali haina mpango wa kufungia watu majumbani mwao na kwamba Mungu aliyeiepusha Tanzania na madhara makubwa ya ugonjwa wa Corona mwaka jana ataiepusha na mwaka huu.