JPM : Enzi za Mwalimu Mafisadi waliingia jela kwa fimbo na kutoka kwa fimbo

0
225

“Kupitia Azimio la Arusha, Baba wa Taifa aliweka misingi na kusimamia vema nidhamu na uzalendo miongoni mwa Watumishi wa Umma, na hakuwa na mchezo na Watumishi waliojihusisha na vitendo vya ubadhilifu na Mafisadi wa mali za umma, yeyote aliyebainika kufanya vitendo kama hivi alikuwa akiingia jela kwa fimbo na kutoka kwa fimbo” Rais John Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, wakati wa Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa.