JPM azindua mtambo wa Gesi

0
386

Rais Dkt. John  Magufuli amesema  serikali  itaendelea kushirikiana  na sekta binafsi katika kuhakikisha nishati ya gesi inasambazwa kwa wingi ndani ya nchi

Akizungumza na wananchi jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua ghala na mtambo ya LPG ya TAIFA GAS, Rais Dkt. Magufuli amesema wakati umefika kwa watanzania kuzalisha gesi kwa wingi.

Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Taifa Gas Mhandisi  Hamisi Ramadhani   amesema  mahitaji ya gesi kwa sasa ni makubwa ndani na nje ya nchi na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mradi huo unakuwa na mafanikio kwa Taifa.

Kampuni ya gesi ya Taifa imeagizwa kusambaza kwa wingi gesi ili kuhakikisha inapatikana  nchi nzima na kuwataka watanzania kutumia gesi hiyo ambayo matumizi yake ni nafuu.