Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametuma salamu za pole kwa Rais Uhuru Kenyatta na Wakenya wote kufuatia kifo cha Rais Mstaafu, Daniel Arap Moi.
Rais Magufuli amesema Watanzania watamkumbuka Rais Moi kwa uongozi wake mahiri, jitihada za kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya, na kufufua Jumuiya ya Afrika Mashariki.