JPM asema hakuna corona nchini, asisitiza kuchukuliwa kwa tahadhari

0
224

Rais John Magufuli ameziagiza mamlaka zinazohusika kutoa elimu kwa Wananchi ya namna ya kujikinga na virusi vya corona.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati akizindua karakana kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hata hivyo Rais Magufuli amesisitiza kuwa virusi vya corona havijaingia nchini, lakini tahadhari ni muhimu.

Amewaelekeza viongozi wa ngazi zote wakiwemo wale wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanaandaa utaratibu mzuri utakaowawezesha wanaowaongoza wanapata taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa virusi vya corona.

Hivi karibuni, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa taarifa yake inayosema kuwa katika siku chache zijazo virusi vya corona vitasambaa katika nchi nyingi zaidi duniani na kusababisha vifo, na kutaka kuchukuliwa kwa hatua za dharura za kukabiliana na virusi hivyo.