JPM aendelea na ziara Songwe, awake jiwe la msingi ujenzi wa barabara

0
282

“Maendeleo yana gharama zake, ukijenga ndani y a barabara umekwenda kutafuta umaskini, ukitaka kuwa maskini nenda ukajenge kando ya barabara, na ndio maana hiyo hospitali nimecheki leo naangalia hizo mita 30 kama zimefika nikaona imefika iko nje ya mita 30, ingekuwa iko ndani ya barabara ningesema ibomolewe hapa hapa leo” Rais John Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Mpemba-Isongole yenye urefu wa Kilometa 50.3, ikiwa sehemu ya ziara yake kikazi ya siku Nne mkoani Songwe.

Rais ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kumsimamia Mkandarasi anayejenga barabara hiyo, kwa kuwa amechukua muda mrefu kukamilisha ujenzi.

Rais Magufuli pia ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospitali ya mji wa Tunduma mkoani Songwe, na kumpongeza Mkandarasi anayetekeleza mradi huo ambaye ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kufanya kazi nzuri.