JPM aeleza alivyompata Majaliwa

0
257

“Wakati natafuta Waziri Mkuu nilipata shida sana, lakini siku ya mwisho likanijia jina la Majaliwa na kwa kweli anafanya kazi sana ya kuwatumikia Wananchi”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akihutubia Mamia ya Wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Likangala wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ambapo ni nyumbani kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa alikua akihitaji Msaidizi wa aina ya Majaliwa katika nafasi ya Waziri Mkuu na kweli amempata.

“Kufanya kazi na mimi inahitaji moyo wa kipekee, maana mimi ni mgumu sana, sasa nimeona Mheshimiwa Majaliwa ameweza nampongeza”, amesema Rais Magufuli.