Joseph Magufuli: Mama anaendelea na matibabu

0
698

Joseph Magufuli ambaye ni mtoto wa Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania, amewaomba Watanzania kumuomba Mwenyezi Mungu ili Taifa liendelee kuwa na amani, upendo na mshikamano.

Joseph ameyasema hayo mkoani Dodoma kwa niaba ya familia ya Hayati Dkt Magufuli, wakati wa Kongamano lililoandaliwa na viongozi wa dini ili kumshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya Dkt. Magufuli hapa duniani pamoja na kuwaombea Viongozi wengine waliopo madarakani.

Amesema.familia inawashukuru Watanzania wote na hasa Viongozi wa dini kwa kuombea familia yao wakati wote wa msiba wa Baba yao Hayati Dkt. Magufuli.

Katika salamu hizo, Joseph amesema Mama yake Janeth Magufuli ameshindwa kushiriki katika kongamano hilo kwa kuwa hali yake kiafya sio nzuri na anaendelea na matibabu.

Amesema Mama yao alipata mshtuko baada ya kifo cha Baba yao Dkt. Magufuli.