Joseph Butiku Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere

0
173

Bodi ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere imemteua Joseph Butiku, kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya taasisi hiyo ambapo amekuwa Mwenyekiti wa tatu baada ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na Salim Ahmed Salim.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Butiku amesema atahakikisha wanasimamia misingi iliyoachwa na waasisi wa taasisi hiyo katika kuhakikisha taifa linaishi kwa umoja amani na kazi za maendeleo  ya watanzania zinawanufaisha wananchi.

Butiku  ameteuliwa katika nafasi hiyo baada ya Salim Ahmed Salim kumaliza muda wake huku bodi hiyo ikiwa na wajumbe 10.