Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Temeke, Mrakibu wa Polisi Sule wamefanya ukaguzi katika magari ya abiria ili kuona kama abiria wanafuata miongozo iliyotolewa na wizara ya afya ya kuvaa barakoa wakiwa katika usafiri wa umma.
Akizungumza na abiria pamoja na wahudumu wa mabasi hayo ya abiria Jokate amesema, hatua zinazochukuliwa na Kikosi cha usalama narabarani wilayani humo zinalenga kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19.
Jokate amesema suala la kuvaa Barakoa ni la lazima katika vyombo vya usafiri na kwamba abiria asiyavaa barakoa atateremshwa kutoka katika vyombo vya usafiri.
Wiki mbili zilizopita Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla aliagiza wakuu wa wilaya wote wa mkoa huo kuhakikisha wanasimamia agizo la Wizara ya afya la wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa wakiwa katika vyombo vya usafiri.