Joe Biden ameapishwa kuwa Rais wa 46 wa Taifa la Marekani, katika sherehe zilizofanyika jijini Washington na kuhudhuriwa na watu wachache.
Rais Joe Biden ambaye ndiye Rais wa kwanza mwenye umri mkubwa kula kiapo nchini Marekani, ameapishwa na Jaji Mkuu wa nchi hiyo John Roberts.
Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Rais Joe Biden ametaka kuimarishwa kwa umoja na mshikakano miongoni mwa Raia wa Marekani.
Pia amesema kuwa atakuwa Rais wa Raia wote wa Marekani na ameahidi kuwatumikia kwa usawa.
Joe Biden ameapishwa pamoja na Makamu wake Kamala Harris, ambaye ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.