Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limesema bado kilimo ni uti wa mgongo na tegemeo kubwa nchini, hivyo litaendelea kuweka nguvu kubwa kwa vijana Ili waendelee kuimarisha usalama wa chakula kupitia uzalishaji bora.
Mkuu wa Utawala JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema Jeshi hilo lipo mstari wa mbele kuimarisha uzalishaji, hivyo ni muda mzuri wa vijana kuchangamkia fursa za kilimo.
Brigedia Jenerali Mabena amempongeza Rais Samia Suluhu Hasan kwa kuendelea kuiboresha sekta ya kilimo kwa kutenga bajeti na kuweka mikakati bora kwenye sekta hiyo.
Amesema katika kipindi ambacho Jeshi la Kujenga Taifa linajiandaa na maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, bado linaweka msisitizo wa kuwa kinara katika uzalishaji kupitia kilimo.