Jiwe la msingi la ujenzi wa Ikulu Chamwino kuwekwa kesho

0
428

Rais John Magufuli leo amekagua maandalizi ya sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za Ikulu Chamwino mkoani Dodoma zitakazofanyika hapo kesho.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi hizo litawekwa na Rais Magufuli, Mama Maria Nyerere kwa kwa niaba ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mzee Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete.

Sherehe hizo zitarushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao.