Wananchi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameshiriki katika mazishi ya jino la mwanamapinduzi aliyeshiriki katika kupigania uhuru wa Taifa hilo kutoka Ubelgiji, Patrice Lumumba ambaye aliuawa Januari 16 mwaka 1961.
Mazishi hayo ambayo yamefanyika kwa heshima za kitaifa yakiongozwa na Rais Felix Tshisekedi wa DRC, yamehusisha wananchi mbalimbali wakiwemo ndugu wa mwanamapinduzi huyo.
Wananchi hao wamesema kurejeshwa kwa jino la mwanamapinduzi huyo na kuzikwa kitaifa hakutoshi bila watuhumiwa wa mauaji yake ambao baadhi yao bado wako hai kuchukuliwa hatua za kisheria.