Jeshi la Polisi mkoa wa pwani limepokea msaada wa vifaa vya ujenzi venye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kiwanda cha kutengeneza marumaru cha KEDA kilichopo chalinze mkoani humo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba 24 zinazojengwa na serikali kwa ajili ya kuboresha makazi ya askari .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema msaada huo wa boksi 324 wa marumaru utasaidia ukamilishaji wa nyumba hizo ambazo zinatakiwa kumalizika kabla ya tarehe 30 mwezi huu.
Jeshi la Polisi mkoa wa pwani limepokea msaada wa vifaa vya ujenzi venye thamani ya shilingi milioni tano kutoka kiwanda cha kutengeneza marumaru cha KEDA kilichopo chalinze mkoani humo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba 24 zinazojengwa na serikali kwa ajili ya kuboresha makazi ya askari .
Kamanda wa Polisi mkoa wa pwani wankyo Nyigesa amesema msaada huo wa biksi 324 wa marumaru utasaidia kwa kiasi kikubwa ukamilishaji wa nyumba hizo ambazo zinatakiwa kumalizika kabla ya tarehe 30 mwezi huu.
Kwa mujibu wa kamanda Nyigesa kazi za ujenzi wa nyumza 24 za polisi katika mkoa huo inaendelea kwa kasi kubwa na kwa sasa ziko katika hatua za umaliziaji na uwekeji wa mifumo ya maji. Kwa upande wake afisa utawala wa kiwanda cha Keda Tanzania Frenk Zhang amesema wametoa msaada huo kuunga mkono juhudi za serikali za kunjenga nyumba mpya kwa ajili ya kuboresha makazi ya askari.