Rais John Magufuli amelipatia Jeshi la Polisi nchini jengo la Ghorofa Nne lililopo jijini Dodoma, ambalo litatumika kama Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini.
https://www.youtube.com/watch?v=szNFatTrqpI&feature=youtu.be
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 118 za askari zilizopo eneo la Nzuguni mkoani Dodoma, Rais Magufuli amesema kuwa, ameamua kutoa jengo hilo lilolokuwa mali ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na Jeshi hilo.
