Jeshi la Polisi lajiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu

0
317
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na uhalifu unaovuka mipaka.

Simbachawene amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Wakuu Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi kilichofanyika kwa muda wa siku tatu, kikao ambacho kililenga kufanya tathimini ya utendaji wa kazi za Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga imara kuhakikisha vinaimarisha hali ya usalama hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu huku akiwataka wananchi pamoja na wanasiasa kutimiza wajibu wao kwa kutojiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.