Ujenzi wa jengo la kisasa la huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Meta litaibua Tumaini jipya kwa akina Mama waishio mkoani Mbeya na mikoa Jirani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji wakati akifanya mahojiano na TBC Aridhio.
“Jengo hili halitahudumia mkoa wa Mbeya pekee bali hadi mikoa jirani na kama unavyofahamu tumepakana na nchi jirani kwa hiyo Itatoa huduma kwa upana mkubwa”-amesema Dkt. Mbwanji.
Mapema leo Rais Samia Suluhu Hassan, aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospitali ya rufaa ya Kanda Mbeya iliyopo jijini Mbeya.