Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita lazinduliwa

0
344

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa, mikoa 18 pekee nchini ndiyo yenye majengo ya Mahakama za Hakimu Mkazi huku mikoa mingine ikiwa inatumia majengo ya kukodi

Akizungumza katika uzinduzi wa jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita Profesa Ibrahim Juma amesema kuwa, ujenzi wa miundombinu ya mahakama ikiwa ni pamoja na majengo bado unaendelea katika mikoa mbalimbali nchini

Awali Jaji Kiongozi Dkt Eliezer Feleshi alibainisha kuwa kabla ya kuwepo kwa jengo hilo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, walikua wakilazimika kuendesha kesi katika mkoa wa jirani wa Mwanza na hivyo kusababisha baadhi ya kesi kubwa kuharibika.