Jecha Salum Jecha afariki dunia

0
196

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha amefariki dunia.

Taarifa zinaeleza kuwa Jecha amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati wa uhai wake, jina la Jecha lilijipatia umaarufu mkubwa hasa baada ya kufuta matokeo ya Urais ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgombea wa upande mmoja kujitangazia ushindi.