Jamii yatolewa hofu kuhusu usalama wa chanjo ya UVIKO-19

0
246

Jamii imetakiwa kuachana na mila potofu kwenye masuala ya kitaalam ikiwepo Afya baada ya kuwepo kwa watu kutojitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa madai kuwa inaathili Afya za mtu aliyechanjwa

Hayo yamesemwa na mratibu wa chanjo mkoa wa Arusha Wilson Boniphace wakati wa mafunzo yanayoendelea kutolewa kwa maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa Afya na azaki zinazotoa huduma za Afya ya Jamii Mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na PHEDES Tanzania

Boniphace ameelekeza kuwa kumekuwa na changamoto ya jamii kuingiwa na hofu kunapotokea chanjo mpya huku akiwataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kutoa elimu kwa Jamii zao ili kuinua Ari na mwamko wa watu kujitokeza kwenye vituo vya Afya kwa ajili ya kuchanja.

Mkurugenzi wa PHEDES Tanzania John Ambrose ambaye pia ni mkufunzi wa masuala ya Afya ya Akili ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo amesema viongozi wa Dini waendelee kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa Jamii ili kupata chanjo ili kuwa na Jamii yenye Afya njema ya Akili na saikolojia ya kujitambua

Aidha Ambrose ameongeza kuwa lengo la kuanzisha mafunzo haya ya Afya ya Akili na saikolojia kwa maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa Afya na azaki zinazotoa huduma za Afya ya Jamii Mkoa wa Arusha na Mbeya ni kuwajengea uwezo wa wataalamu hao kuhudumia Jamii kwa ufanisi zaidi.