Jaji Mkuu ataka usuluhishi kutatua migogoro

0
166

Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amesisitiza kufanyika kwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi.

Amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi una faida nyingi ikiwa ni pamoja na mashauri kumalizika kwa haraka na kufanyika kwa njia ya urafiki.

Jaji Mkuu ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini, maadhimisho yanayoashiria kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama.

Amesisitiza kuwa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni chanzo cha watu kuwa wamoja na Taifa kuwa moja.

Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma ametoa pendekezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuliweka suala ya usuluhisi liwe la lazima, jambo ambalo pia litasaidia kupunguza mlundikano wa mashauri katika mahakama.