Jaji Masaju ateuliwa mshauri wa Rais

0
161

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria.

Jaji Masaju ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Uteuzi wa Jaji Masaju umeanza Aprili 20, 2023.

Rais Samia pia amemteua Dkt. Richard Muyungi kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi na Mazingira.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Muyungi alikuwa Meneja wa Mazingira katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Uteuzi wa Dkt. Muyungi umeanza Aprili 19, 2023.