Jaji Iman Aboud Rais mpya wa Mahakama ya Afrika

0
197

Jaji Iman Aboud wa Mahakama Kuu ya Tanzania amechaguliwa kuwa Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu.

Kwa ushindi huo, Jaji Aboud anakuwa Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo baada ya Jaji Augustino Ramadhani aliyeshika wadhifa huo kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2016.

Aidha, amekuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo nyuma ya Jaji Sophia Akuffo aliyeshika wadhifa huo kuanzia mwaka 2012 hadi 2014.

Jaji Aboud amesema ushindi huo ni heshima kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu

Majaji wengine waliokuwa wakigombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon.